UJENZI WA KANISA
UKAMILISHAJI WA UJENZI WA JENGO LA KANISA. KANISA LA WASABATO BUTIMBA, MWANZA.
Hapo juu ni picha zinazoonesha kazi ya ujenzi ikiendelea kwa hatua ya kusuka mbao kwa ajili ya ceiling board. Kama inavyoonekana bado kuna kazi ya kusuka nyaya za umeme, ceiling board, kuweka feni na vigae kwenye sakafu, kupaka rangi ndani na nje ya jengo.
HISTORIA FUPI YA KANISA LA BUTIMBA
Kanisa la Wasabato Butimba ni kanisa la pili kwa kuanzishwa baada ya kanisa la Kirumba katika jiji la Mwanza, jengo lake la kwanza lilikuwa la tofali za tope ambalo lilidumu kwa muda mrefu hadi kufukia hatua ya kuchakaa na hata kutokidhi haja ya kwa washiriki baada ya washiriki kuongezeka. Kanisa hili limekua na kuzaa makanisa ya Igogo, Mkuyuni,Nyegezi, Sweya, na Tambuka reli.
JIOGRAFIA YA KANISA
Kanisa hili lipo uelekeo wa kusini mwa mji wa Mwanza, pembezoni mwa barabara ielekeayo Gereza la Butimba na Chuo cha Ualimu Butimba kwenye mwinuko wa kilima kidogo cha mtaa wa Sungwa. Umbali kutoka barabara ya Shinyanga (Shinyanga road) ni takribani ya kilomita moja.
OMBI
Idara ya Majengo kwa niaba ya uongozi wa Kanisa inawaomba washiriki na marafiki wapendwa kuendelea kutoa michango ili kukamilisha ujenzi huu.
0 comments: