SAUTI KUU AU KILIO KIKUU CHA MWISHO
imeandaliwa na Mch. Kenani Mwasomola, Uwakili - SHC
Fungu kuu: Ufunuo 18:1 – 5. “Baada ya hayo naliona Malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, umeanguka maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza, kwa kuwa mataifa yote yamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake”
Utangulizi: Neno malaika, ambalo kwa kiyunani ni “angelosi” humaanisha mjumbe au taarishi. Neon hili limetumiwa sana katika kitabu cha Ufunuo. Mahala pengine limetumiwa kumaanisha malaika wa Mungu watokao juu. Hawa nao ni wajumbe wa Mungu waletao habari njema kutoka juu mbinguni kwa wanadamu. Lakini pia wanadamu wanaomwamini Yesu na kupeleka injili ya wokovu kwa wanadamu wenzao nao hujulikana kama Malaika – wajumbe wa Bwana.
MALAIKA WA KILIO KIKUU: katika Ufunuo 14:8 ujumbe wa malaika wa pili unasikika “---- umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.
Je Babeli anayetajwa kwamba umeanguka ni nini? Babeli kwangu kabisa humaanisha machafuko. Babeli ni kanisa la kiulimwengu na lililoenea ulimwenguni kote. Babeli imeyafanya mataifa yote kunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake ambayo ni mafundisho ya uongo yaliyo kinyume na neno la Mungu. Hivyo Babeli huwakilisha kanisa la kidunia tu.
Uriah Smith, The prophecies of Daniel end the Revelation (Washington, DC: Review and Herald Publishing Association, 1994) pg. 646 – 7.
Babeli ule mji mkubwa unaundwa na makundi matatu. Hivyo dini kubwa ya dunia hii zinaweza kupangwa katika vichwa vitatu:
- ya kwanza na ya zamani sana na iliyoenea sana ni upagani (ukafiri yaani ushenzi) unawakilishwa na joka.
- Ya pili ni uasi mkubwa wa upapa, unawakilishwa na mnyama.
- Ya tatu ni mabinti(makanisa yanayofuata uasi wa upapa) au wazao wa kutoka kanisa la Rumi ya kiroho, yakiwakilishwa na mnyama mwenye pembe mbili, ingawaje hiyo haichukui yote.
Vita, mateso, unafuatisha namna ya dunia hii, mtindo wa kidini ibada ya (mali), kutafuta anasa, na kudumisha kila kosa la kanisa katoliki, kwa huzuni hudhihirisha makanisa ya Kiprotestant kuwa sehemu muhimu ya Babeli mkuu 2. Ujumbe wa unaanguka kwa Babeli ulitolewa kwa mara ya kwanza mnamo 1844 na wanamarejeo watu walioamini kuwa Yesu angerudi mnamo 22 Oktoba 1844. Huu ujumbe ulikuwa ni onyo kwa watu ambao walikanusha na kupinga ujumbe wa marejeo ya Yesu Kristo. Ujumbe huo utarudiwa tena kwa usahihi kabisa na malaika mwingine ambaye awafuata wale malaika watatu wa Ufunuo 14:6 – 12. ujumbe wa malaika wa Ufunuo 18:1 – 5 utatolewa kwa nguvu ya mvua ya masika Roho Mtakatifu atakayemwagwa kwa wingi juu ya watu wa Mungu walio waaminifu katika kufuata neno la Mungu na wenye imani ya Yesu.
Watu wa Mungu, wakiwa wamejazwa Roho Mtakatifu (Mvua ya masika) watasonga mbele kwa nguvu wakitoa mwito kwa watu walioko katika Babeli ili watoke kurudi wasije wakashiriki maangamizo yake yaliyo ya hakika. [Uriah Smith, The Prophecies of Daniel and the Revelation, P. 647.]
Yohana anaandika kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake (Ufunuo 18:4 – 5) “---- ujumbe wa malaika wa tatu utatangazwa kwa uweza mkuu na wale wanaotoa onyo la mwisho dhidi ya mnyama na sanamu yake” (8T 118). Matangazo hayo, yakiungana na ujumbe wa malaika wa tatu yanakuwa sehemu ya onyo la mwisho litakalotolewa kwa wakazi wa dunia hii (GC 604). “WATU WA Mungu ambao bado watakuwa Babeli wataitwa ili wajitenge na ushirika wake. Ujumbe huu ndio wa mwisho ambao utapata kutolewa kwa ulimwengu” (GC 390)
Watu maelfu kwa maelfu watatoka kutoka katika Babeli na kujiunga na watu wa Mungu na Mungu atatia muhuri wake juu yao.
MAIGIZO YA SHETANI KABLA YA KUTIMIZWA KWA UFUNUO 18:1
Mjumbe wa Mungu, Ellen G. White anasema ya kwamba, Adui wa roho za watu anataka kuzuia kazi hii, na kabla ya wakati wa vuguvugu kama hilo kuja, atajitahidi kulizuia kwa kuleta uamsho wa bandia. Katika yale makanisa ambayo naweza kuyaleta chini ya uwezo wake wa madanyanyo atafanya ionekane kuwa mbaraka pekee wa Mungu unamwagwa juu yao, kutaonekana kila kinachodhaniwa kuwa ni mwamko mkubwa wa mambo ya kidini. Makutano ya watu watashangilia wakisema kwamba Mungu anatenda maajabu kwa ajili yao, wakati kazi hiyo ni ya roho yule mwingine. Akiwa amejificha chini ya vazi la dini, shetani atajaribu kuueneza ushawishi wake katika ulimwengu wote wa Kikristo (GC 464)
Kila siku watu wanasikia na pengine hata kushuhudia maajabu yanayofanywa kwa jina la Yesu lakini kwa undani wake hasa maajabu hayo yanafanywa kwa uwezo wa adui Ibilisi. Katika siku hizi za mwisho shetani, kupitia watumishi wake, atafanya ishara kubwa za uponyaji na hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye atawakosesha wale wakaao juu ya nchi kwa ishara zile alizopewa kuzifanaya (Ufunuo 13:13,14). Watu wengi watakoseshwa kwa ishara hizo na maajabu hayo. Lakini watu wa Mungu kamwe hawatashibishwa. Daima wao watakumbuka, hata ishara kubwa na maajabu yasiyo ya kawaida yatakapotendeka mbele ya macho yao, neno lao ni moja tu, imeandikwa na waende kwa sheria na ushuhuda, ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, kama mtu anayefanya ishara za uponyaji, unenaji wa lugha, kufufua watu au hata kushusha moto kutoka juu mbinguni, hashiki amri za Mungu na wala hana ushuhuda wa Yesu ambao ni Roho ya unabii(Ufunuo 19:10) huyo mtu hakutumwa na Mungu na roho itendayo kazi ndani yake siyo ya Mungu. Watu wa Mungu washikao amri za Mungu (Ufunuo 14:12)nao watafanya ishara na miujiza. Lakini daima watakumbuka kuwa imani yao haikujengwa juu ya miujiza na maajabu bali imani yao imejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. (Waefeso 2:20)
TUWEZAJE KUPAMBANUA KATI YA UAMSHO BANDIA WA SHETANI NA SAUTI KUU?
Mjumbe wa Mungu, anaweka bayana ya kwamba katika uamsho bandia, kuna msisimuko wa kihisia kuchanganya ukweli na uongo, ambavyo vimekusudiwa kuwapotosha watu. Hata hivyo, hakuna haja kwa yeyote kudanganyika. Katika nuru ya neno la Mungu si vigumu wanapodharau ushuhuda wa Biblia, wakigeukia na kuziacha zile kweli zilizo dhahiri na zenye kuupima moyo na ambazo zinahitaji kujikana nafsi na kuukataa kabisa ulimwengu, hapo ndipo tunapoweza kuwa na uhakika ya kwamba mbaraka wa Mungu, haujatolewa. Na kwa kanuni ile aliyoitoa Kristo mwenyewe, mtawambua kwa matunda yao (Mathayo 7: 16),ni dhahiri kwamba vuguvugu hilo siyo kazi ya Roho wa Mungu (GC 464, 465)
Je Ni lini ambapo anguko la Babeli (Ufunuo 18:2) litakuwa limetimilika hata Ufunuo 18:2 liweze kuhubiriwa kama uliotimia kabisa? “ uliowanywesha mataifa, yote mvivyo wa ghadhabu ya uasherati wake” (Ufunuo 14:8) Mafundisho ya uongo. Jambo hilo linafanyikaje? Kwa kuwalazimisha watu kuikubali sabato ya uongo(8T 94) Jumapili ndiyo sabato ya uongo. Ni mpaka hapo hali hiyo itakapofikiwa na muungano wa kanisa lna ulimwengu utakapokamilika anguko la Babeli litakapokuwa limekamilika. Badiliko ni la kuendelea, na utimizo kamili wa ufunuo 14:8 bado uko siku za usoni (GC 390).
Kupitishwa kwa amri ya Jumapili kutakuwa ndiyo mwanzo wa taabu na mateso.Lakini “mwanzoni mwa wakati wa taabu, tulijazwa na Roho Mtakatifu tulipoondoka kwenda kuitangaza Sabato kwa ukamilifu zaidi” (EW 33, NA 85). “Sabato hiyo ya uongo italazimishwa kwa sheria ya ukandamizaji. Shetani na malaika zake wako macho sana, tena wanashughulika kwa nguvu sana -----. Lakini wakati shetani atakapofanya kazi kwa maajabu yake ya uongo, ndipo utakapotimizwa wakati uliotabiriwa katika Ufunuo, na malaika yule mwenye mamlaka kuu atakayeitangaza dunia yote kwa utukufu wake, atatangaza anguko la Babeli, na kuwaita watu wa Mungu walioko huko watoke (7BC 985, RH 13/12/1892).
SAUTI KUU ITAFANANA NA PENTEKOSTE.
Kazi hiyo itafanana na ile ya siku ya pentekoste. Kama vile mvua ya vuli iliyotolewa kwa kumwaga Roho Mtakatifu mwanzoni mwa kazi ya injili ili kusababisha kuchipua kwa mbegu zile za thamani, ndivyo “ Mvua ya masika itakavyotolewa mwishoni ili kukomaza mavuno” (GC 611)…“Kumwagwa kwa Roho katika siku za mitume ilikuwa ni mvua ya vuli, na matokeo yake yalikuwa ya utukufu sana. Lakini mvua ya masika itakuwa nyingi zaidi” (Ev 701).
Je, watoto wa Mungu ambao bado watakuwa Babeli wataupokea mwito wa sauti kuu? Jawabu ni ndiyo. Mjumbe wa Mungu Ellen White anasema, Roho zilizokuwa zimetawanyika katika mashirika yote ya kidini ziliitikia mwito na zile zilizokuwa za thamani ziliharakishwa kutoka katika makanisa yakwenda kuangamizwa, kama vile Lutu alivyoharakishwa kutoka Sodoma kabla ya maangamizi yake(EW 279). Hakuna chochote kitakachoweza kuwazuia wabakie Babeli. Mahusiano ya kifamilia, mahusiano ya kikanisa, sasa hayana uwezo wowote wa kuwazuia. Ukweli ni wa thamani zaidi kuliko mengine yote.Bila kujali mawakala walioungana dhidi ya ukweli, idadi kubwa ya watu, watachukua msimamo wao upande wa Bwana. (GC 612).
WAADVENTISTA WASABATO AMBAO HAWAJAONGOKA.
Jambo la kusikitisha, Waadventista wa Sabato ambao hawajaongoka hawatatambua sauti kuu na wataipinga kazi hiyo. White anasema kuwa “kutakuwa na udhihirisho wa ajabu wa uweza wa Mungu katika makanisa yetu, lakini uweza huo hautawajia wale ambao hawajajinyenyekeza wenyewe mbele za Bwana, na kuifungua mioyo yao kwa maungamo na toba katika udhihirisho wa uweza unaoiangaza dunia yote kwa utukufu wake, wao wataona tu kuwa ni mila fulani ambacho katika upofu wao watafikiria kuwa ni cha hatari, kitu fulani kitakachoamsha hofu zao, nao watajidhatiti kuupinga kwa kuwa Bwana hafanyi kazi yake kulingana na matarajio na mawazo yao, basi, wataipinga kazi hiyo. Watasema “kwa nini sisi tusiweze kumjua Roho wa Mungu wakati tumekuwa kazini kwa miaka mingi sana?” RH 7/11/1918…. “Dhoruba inapozidi kukaribia, kundi kubwa la wale wanaodai kuwa na imani katika ujumbe wa malaika wa tatu lakini ambao hawakutakaswa kwa kuitii ile kweli, wataziacha nafasi zao na kujiunga katika safu za wapinzani” (GC 608)
Huu ndio wakati wa kila mmoja kuchukua msimamo thabiti kuwa upande wa Bwana. Wale wanongojea wakati fulani wa pekee ambamo watategemea tabia zao kugeuka ghafla na kuwa kama Kristo, wakati huo hawataupata. Leo hii ndivyo nafsi na wakati wa kupata mvua ya vuli (Roho Mtakatifu wa kwanza) tayari kwa kupokea mvua ya masika yaani Roho Mtakatifu atakayemwagwa bila kipimo wakati wa mwisho na atayewawezesha malaika wa Ufunuo 18:1 – 5 kupeleka ujumbe wa onyo la mwisho kwa kishindo kikubwa sana.
“Wakati uweza wa Mungu utakapounganishwa na juhudi za binadamu, kazi itaenea kama moto katika nyasi kavu zilizokatwa Mungu atatumia mawakala ambao asili yao mwanadamu hataweza kuifahamu, malaika watafanya kazi ambayo wanadamu wangeweza kupata mibaraka ya kutimiza, kama wasingepuuzia kuitikia madai ya Mungu” (RH 15/12/1885)
Mambo makuu ya kufanya ili kujiandaa kwa wakati huo wa mwisho:-
- Soma neno la Mungu (Biblia) kila siku
- Omba bila kukoma. Uwe na maombi ya mnyororo katika maisha yako yote.
- Fanya kazi ya kuihubiri Injili waweza kuhubiri kwa njia ya kupeleka vitabu, sauti ya unabii, Biblia yasema, masomo ya mgunduzi, mahubiri ya hadhara, kuonana kuombea wagonjwa hospitalini na majumbani n.k. Mungu atatungoja sisi kama watu wake tuweze kuifanya kazi yake kwa mali, nguvu, na akili zetu.
Wito: ni nani basi ajitoaye kwa moyo ili ajiweke wakfu kwa Bwana? (1Nyakati 29:5)
SOMO LA NNE.
DHIKI KUU
imeandaliwa na Mch. Ezekia Chaboma, Uchapaji - SHC
FUNGU KUU: Matendo 16:16-18
UTANGULIZI
Katika siku hizi za hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya miujiza kwa njia ya shetani na hata watu wengi na miongoni mwa Wa Adventista wamepata kushawishika na hata kuamini baadhi ya miujiza kama hiyo. Biblia inasema yamkini hata walio wateule watachanganywa na hiyo miujiza.
Nguvu ya umizimu imebadili mbinu zake za kutenda kazi. Mwanzoni umizimu ulimkataa kabisaYesu, haukutenda shughuli zake kwa jina la Yesu. Lakini leo wapo watu wengi sanawanaotenda hiyo miujiza kwa jina la Yesu na hivyo kuwafanya wengi kuamini kuwa hiyo ni kazi ya Mungu wakati sivyo bali ni kazi ya yule Mwovu.
Ø Wagonjwa wanaponywa
Ø Watu wanapata utajiri wa haraka haraka
Ø Watu wanadai wameoneshwa maono.
SOMO
IMANI YA UMIZIMU ILIANZA TANGU ZAMANI
Ø Wachawi wa Misri walibwaga fimbo zikawa nyoka (Kutoka 7:8-13)
Ø Mungu alitoa Agizo kwa wana wa Israel kuwa wasiende kwa Wachawi (Walawi 20:6,27) Adhabu ya kifo ilitolewa kwa wote waliojulikana kuwa ni wachawi.
Ø Wakati wa Yesu pia kulikuwa na miujiza ya kishetani na mapepo. (Marko 5:1-18) kuponywa kwa yule mwenye pepo wengine walichukia maana nguruwe wao walizama baharini.
NINI KINATOKEA UMIZIMU UNAPO TAWALA
Katika kitabu cha Dhiki kuu Uk. 61 “Roho wa Mungu anaondoka hatua kwa hatua ulimwenguni. Shetani naye pia anakusanya majeshi yake ya uovu, akiwaendea wafalme wa dunia na wa ulimwengu wote, kuwakusanya chini ya bendera yake, ili kuwapa mafunzo kwa ajili ya “Vita ya siku ile kuu ya Mungu mwenyezi” …“Chini ya uongozi wa pepo hao wachafu, watu watafanya miujiza. Watawafanya watu kuwa wagonjwa kwa kuwatupia uchawi, kisha watauondoa na kuwafanya watu wengine kusema kwamba wale walio kuwa wagonjwa wameponywa kimiujiza. Jambo hilo shetani atalifanya tena na tena. Uk. 62, 63.
Si jambo la kuamini ikiwa watu wachache kuwa watoa uponyaji lakini wanakana nguvu za Mungu. Isaya anasema “Nawaende kwa sheria na ushuhuda….” Isaya 20:8
Siku za hivi karibuni wametokea watu wakifanya miujiza (Muujiza wa kikombe cha Babu – Loliondo) Mamia kwa maelfu ya watu wameenda kunywa hicho kikombe. Je! Hizo nguvu za uponyaji za tokana na Mungu? Je, upo ushirikiano wowote kati ya nuru na giza?
Huu ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwa baadhi ya Waadventista wasabato.Maana baadhi walishawishika kwenda na wengine walienda kabisa japo wengi hawakutaka kusema. Ikiwa jaribu hili dogo limewatikisa wengi vipi yatakapokuja yale makubwa watakapoona shetani akishuka toka mbinguni kama Yesu. Kwani kwa muda mrefu walikutazamia kuja kwake. Wengi wataiacha imani.“Pambano litaendelea kuwa kali na kali zaidi. Shetani atachukua uwanja na kuja katika umbile la Kristo. Atakielezea vibaya, atakitumia vibaya, na kupotosha kila kitu kwa kadri atakavyoweza ili kuwadanganya, yamkini, hata walio wateule” Dhiki kuu, Uk. 70.
Biblia katika kitabu cha Luka 17:23 Yesu anasema mkisikia wakisema yuko huko au kule ‘Msiwafuate’ “Ikiwa wanapotoshwa sasa, je watasimamaje wakai Shetani atakapokuja katika umbile la Kristo, na kufanya miujiza?”
SWALI LA MSINGI NI HILI TUTASIMAMAJE KATIKA KIPINDI HICHO KIGUMU?
Nabii anasema katika Dhiki kuu: “Nendeni kwa Mungu ninyi wenyewe, ombeni mpate kuelimishwa na mbingu, ili mpate kujua hakika ya kuwa mnaujua ukweli, ili kwamba wakati uwezo wa Shetani ufanyao miujiza ya ajabu utakapodhihirishwa, na huyo adui kuja kama Malaika wa nuru, muweze kubainisha kati ya matendo ya kweli ya Mungu na matendo ya kuigiza ya nguvu za giza.” – UK. 74.
Hapa ninachambua mambo makubwa MAWILI:
- Twende kwa Mungu sisi wenyewe.
- Tuombe kuelimishwa na mbingu
- Tutapambanua nuru na giza
- Tutabainisha ukweli na uongo
- Tutabainisha miujiza ya kweli na uongo
Hiki ni kipawa cha Roho Mtakatifu. Tutakapompokea hatutaendelea kutenda dhambi. Tutaukana uovu na ubaya wote wa Shetani.
0 comments: